Watu 12 wamenyongwa Pakistan

Pakistan imewanyonga watu kumi na wawili kutoka magereza tofauti kote nchini. Ni idadi kubwa ya mauaji kutekelezwa kwa siku moja tangu ser...

Pakistan imewanyonga watu kumi na wawili kutoka magereza tofauti kote nchini.
Ni idadi kubwa ya mauaji kutekelezwa kwa siku moja tangu serikali iondoe marufuku ya hukumu hiyo kuu mnamo mwezi Desemba.

Pakistan imewanyonga takriban watu arobaini tangu kuanza tena kutumika hukumu hiyo kufuatia shambulio la Taliban dhidi ya shule moja huko Peshawar ambapo watoto wapatao 150 waliuawa.
Serikali imesema kuwa,asilimia kubwa ya waathiriwa ni watu waliopatikana na hatia ya ugaidi mauaji na makosa mengini kama uhaini.

Msemaji wa wizara ya waswala ya ndani ,amesema kuwa takriban watu 8000 wamehukumiwa kinyonga nchini humo.

Aidha wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu wanasema kuwa asilimia kubwa ya hukumu hizo haziwezithibitishwa iwapo ilitimiza vigezo vya kimataifa vya haki kwa watuhumiwa.

-BBC

Related

Habari 4004699705140338112

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item