HUYU NDIE NALIMI MAYUNGA MSHINDI AIRTEL TRACE MUSIC STARS...

Mshindi wa Airtel Trace Music stars NALIMI MAYUNGA PICHA:NA LIVINGSTONE MINJA meneja uhusiano AIRTEL bw. Jackson MMbando PICHA:NA ...

Mshindi wa Airtel Trace Music stars NALIMI MAYUNGA
PICHA:NA LIVINGSTONE MINJA
meneja uhusiano AIRTEL bw. Jackson MMbando
PICHA:NA LIVINGSTONE MINJA
Kampuni ya simu za mikononi ya airtel imetoa wito kwa watanzania na wapenda burudani kwa ujumla kumpigia kura msanii chipukizi NALIMI MAYUNGA ili arudishe heshima ya ushindi nyumbani katika fainali za airtel trace music stars Nairobi machu 28 mwaka huu 2015 katika hoteli maarufu ya Enashipai iliopo jijini humo

Mayunga akiwa na timu ya airtel katika mkutano na waandishi
leo jijini dsm
PICHA:NA LIVINGSTONE MINJA


akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm . Meneja masoko wa airtel Tanzania bi Aneth Muga amesema Mayunga ni msanii mzuri mwenye uwezo mkubwa hivyo ni jukumu la watanzania wote kwa ujumla kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha anarudi nyumbani na taji hilo.


Kwa upande wa meneja uhusiano wa airtel bw. Jackson Mmbando alielezea jinsi ili ilivyo rahisi kumpigia kura Mayunga ambapo ni kutuma SMS yaani ujumbe mfupi wenye neno YUN kwenda namba 15594
pia unaweza kupiga simu 0901002233 hii itakuwezesha kusikiliza nyimbo na waimbaji wote ili kuchagua nani wakumpigia kura.
meneja masoko AIRTEL bi JANETH MUGA
PICHA:NA LIVINGSTONE MINJA


Nchi nyingne 13 zinazoshiriki mashindano hayo barani africa ni pamoja na KENYA, UGANDA, ZAMBIA, MADAGASKA, MALAWI,NIGERIA, GHANA, BURKINA FASO, CHAD, CONGO BRAZZAVILLE, DRC CONGO, NA GABON
pamoja na zawadi nyingine pia Mshindi katika shindano hilo atapata nafasi ya kurekodi nyimbo zake akiwa na msanii nguli wa kimataifana katika studio za kimataifa nchini marekani.
msanii AKON anatarajiwa kuwa mgeni wa heshma katika shindano hilo


Nae MAYUNGA amesema kuwa watanzania wategemee mambo makubwa kwani anajiamini na amejiandaa vyema kuhakikisha analeta heshima nyumbani hivyo amesisitiza watanzania kuonyesha moyo na ushirikiano kama ule waliompa wakati wa mashindano ya hapa nchini na hatimaye kumfikisha hapo alipo.

MUNGU IBARIKI TANZANI.. MUNGU MBARIKI MAYUNGA

Nalimi Mayunga akisisitiza watanzania kumpigia kura katika shindano hilo
PICHA:NA LIVINGSTONE MINJA


Related

Burudani/Michezo 2578044130746400798

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item