Umoja wa Azaki za vijana wazua pingamizi

Umoja wa Azaki za vijana hapa nchini  umepinga vikali juu ya rafu za mchakato wa kuunda Baraza la vijana la Taifa, udhaifu wa maudhui ya m...

Umoja wa Azaki za vijana hapa nchini  umepinga vikali juu ya rafu za mchakato wa kuunda Baraza la vijana la Taifa, udhaifu wa maudhui ya muswada wa Serikali wa sheria ya Baraza la vijana la Tanzania wa mwaka 2015 unaotaka kupitishwa bungeni  kinyemela tarehe 31 machi,2015.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mratibu Azaki za Vijana Bw. DICKSON KAMALA amesema wameshangazwa na kitendo cha serikali kuibua muswada mpya ambao ulichapwa katika gazeti la Serikali la tarehe 9 januari,2015 ambao ni tofauti na muswada binafsi wa mwaka 2013 waliouchambua na kuutolea maoni.

Kwa upande wake Afisa wa Ushauri wa Utetezi Bw. SELEMANI MAKWITA amesema vijana wanahitaji kuwa na baraza  huru ambalo  litalinda na kutetea maslahi ya vijana  kwa taifa hili .

Mwanaharakati wa masuala ya Vijana nchini BW. NAMALA SAMSON amesema baraza huru la vijana linaunganisha vijana wote bila ya kujali itikadi za kidini, kabila wala chama na kuongeza kuwa mswada huo unapaswa uende katika njia sahihi.

Related

Habari 6951773216245051691

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item