Serikali hairisha Kura za maoni_JUKATA
Jukwaa la Katiba Tanzania {JUKATA} limependekeza serikali kuahirisha zoezi la kura ya maoni mpaka mwakani kutokana na kuwepo kwa joto la u...
https://mzukatz.blogspot.com/2015/03/serikali-hairisha-kura-za-maonijukata.html
Jukwaa la Katiba Tanzania {JUKATA} limependekeza serikali kuahirisha zoezi la kura ya maoni mpaka mwakani kutokana na kuwepo kwa joto la uchaguzi mwaka huu 2015.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kaimu Mwenyekiti JUKATA BW. HEBRON MWAKAGENDA amesema hadi kufikia sasa mchakato wa kura ya maoni umepoteza mueleko kwa kuwa uandikishaji wake unafanyika kwa kusuasua.
Aidha Bw. MWAKAGENDA amesema Siku zilizosalia kwa ajili ya kukusanya kura ya maoni hazitoshi kutokana na kuwepo dalili za kukwamisha kura ya maoni kutokana na kauli za viongozi kutofautiana kuhusu ukusanyaji wa maoni hayo.
Katika hatua nyingine Jukwaa la Katiba limeitaka Serikali kuacha kuingilia utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura badala yake itekeleze jukumu la kuwezesha upatikanaji wa fedha za kutosha kwa ajili ya zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa ukamilifu wake.
Hata hivyo Bw. MWAKAGENDA ameongeza kuwa katika mwaka wa uchaguzi kama huu, jambo muhimu linapaswa kuwa uwezeshaji wa elimu ya uraia na elimu ya mpiga kura ya kutosha ili watanzania wajue thamani ya kura yao na kuitumia haki yao kwa kujitambua muda utakapofika.
kaimu mwenyekiti wa JUKATA Bw. Hebron Mwakagenda |