NIMR yaelezea mafanikio yao ya miaka 35

Katika kusherehekea miaka 35 tangu kuanzishwa kwake,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR)imefanikiwa kufanya tafiti nne...

Katika kusherehekea miaka 35 tangu kuanzishwa kwake,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR)imefanikiwa kufanya tafiti nne zinazohusu magonjwa ya binadamu.
Mkurugenzi mkuu NIMR Dr Mwale Malechela

Hayo yamesemwa jijini DAR ES SALAAM na mkurugezi mkuu wa NIMR DR.MWALE MALECHELA wakati akizungumza na waandhishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 35 ya taasisi hiyo.

Aidha DK.MWALE   amesema kuwa taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1980 imefanya utafiti wa  magonjwa  makubwa yanayoikabili  jamii ya kitanzania ambapo utafiti huo umewasaidia kubuni dawa bora  zaidi za magonjwa hayo kama dawa mseto ya malaria na dawa ya  kupunguza makali ya Ukimwi ARVS na kuongeza chembechembe za CD4.

Dokta MWALE ameongeza kuwa Tafiti hizo zimesadia kujengwa kwa Maabara kubwa za kisasa na zenye  usalama katika daraja la 1-3 zenye uwezo wa kuchambua vimelea vya magonjwa katika kundi la mikrobiolojia, parastolojia pamoja na protologia.


_Elia Sebastian

Related

Habari 2607944879576759663

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item