TGNP kuzindua rasmi kampeni ya kuenzi wanawake... soma hapa

Katika kutambua mchango wa wanawake katika jamii Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na wadau wengine wa...

Katika kutambua mchango wa wanawake katika jamii Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na wadau wengine wanatarajia kuzindua kampeni ya kutambua na kuenzi michango ya wanawake katika maendeleo na historia ya nchi kabla,wakati na baada ya uhuru.
Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Bi LILIAN LIUNDI

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Bi.LILIAN LIUNDI amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwaenzi wanawake wote waliofanya vizuri katika kuleta maendeleo nchini.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mkuu wa makumbusho ya taifa Bi.ADELAIDE SALLEMA wao kama wanachama wa baraza la makumbusho duniani wana mchango mkubwa katika kampeni hiyo hivyo amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kampeni hiyo ambayo ni ya kwanza tangu taifa kupata uhuru.

Kampeni hiyo itakayozinduliwa tarehe 27,machi 2015, itavunja kuvunja ukimya kuhusu kutambua na kuthamini michango ya wanawake Tanzania huku akiihamasisha jamii kushiriki katika uzinduzi wa kampeni hiyo  ambayo itawainua wanawake nchini.


_Praygod Thadey

Related

Habari 8025188612316885332

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item