KIKWETE kutoa tuzo ya jamii

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta JAKAYA MRISHO KIKWETE anatarajiwa kuongoza hafla ya utoaji wa tuzo ya jamii itakayofanyika ...

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta JAKAYA MRISHO KIKWETE anatarajiwa kuongoza hafla ya utoaji wa tuzo ya jamii itakayofanyika april 13 mwaka huu katika ukumbi wa mwalimu nyerere jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa kampuni ya Tanzania Awards International ambao ndio waandaaji wa tuzo hiyo  BW.DEONATUS MALEGESI amesema tuzo hiyo inawalenga watu binafsi,taasisi na baadhi ya viongozi ambao wametoa mchango wao kwa jamii.

Aidha BW.MALEGESI amesema kuwa zoezi la kuwapigia kura washiriki limeshaanza huku akiongeza kuwa washiriki watapiguiwa kura kutokana na vipengele vyao na kutoa wito kwa viongozi mbali mbali kufuatilia ushiriki wao katika tovuti ya kampuni hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo chaa utafiti wa kampuni hiyo injinia SYLVESTER MAYANGA amesema tuzo hiyo inalenga kukumbuka na kutathmini michango ya watu mbali mbali nchini katika kutetea maslahi ya jamii husika hivyo kamati ya tuzo ya jamii itatangaza majina ya washindi wa tuzo hiyo kwa kuzingatia utafiti walioufanya na zoezi la upigaji kura.







Related

Habari 670418397748208953

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item