Biashara ya watu wenye Albinism yavuka mipaka... kumbe ni ya kimataifa

Imeelezwa kuwa matukio ya mauaji ya watu wenye ALBINISM  albino si tatizo la TANZANIA bali ni tatizo linalozikumba nchi nyingi za AFRIKA ...

Imeelezwa kuwa matukio ya mauaji ya watu wenye ALBINISM  albino si tatizo la TANZANIA bali ni tatizo linalozikumba nchi nyingi za AFRIKA hasa zilizo kusini mwa jangwa la sahara.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisisi ya UNDER THE SAME SUN Bi.VICKY NTETEMA amewaambia wadau jijini DAR ES SALAAM na kuongeza kuwa chanzo kikuu cha mauaji hayo ni kukosekana kwa elimu juu ya albinism na imani za kishirikina.

Amesema kwa mujibu wa ripoti aliyoitoa kuanzia mwaka 2009 inaonyesha matukio ya kuuawa na kukatwa viungo kwa watu wenye albinism  AFRIKA yamekuwa yakitokea katika kipindi cha kuelekea uchaguzi kutokana na imani za kishirikina zinazohusisha  baadhi ya wanasiasa na waganga wa kienyeji.

Aidha BI NTETEMA amesema kuwa biashara ya viungo vya watu wenye albinism  inayoongoza nchini TANZANIA kwa sasa imekuwa ni biashara inayovuka mipaka kwa kuwahusisha waganga wa kienyeji kutoka nchi mbali mbali hali ambayo imechangia kuongezeka kwa mauaji,utekaji na ukataji viuongo vya watu wenye albinism.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) BISWALO MGANGA amesema kama watanzania wataunganisha nguvu zao katika kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye albinism TANZANIA sehemu salama ya kuishi huku akitoa wito kwa jamii kutoa taarifa za watu wanaojishughulisha na biashara hiyo ili wachukuliwe hatua.





Related

Habari 6210468426220417776

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item