Zaidi ya wakulima 9979 wanufaika na MKURABITA

Zaidi ya wakulima 9979 kutoka mkoani KAGERA katika wilaya za NGARA,KARAGWE na MISENYI wamefaidika na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na B...

Zaidi ya wakulima 9979 kutoka mkoani KAGERA katika wilaya za NGARA,KARAGWE na MISENYI wamefaidika na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).


Akijibu maswali ya wabunge mjini DODOMA jana asubuhi,Waziri wa Kilimo na Ushirika BW.STEVEN WASSIRA amesema mpango huo ulioanza mwaka 2004 umenufaisha zaidi wakulima na bado serikali inaendelea kuboresha mpango huo ili kuwafikia wakulima wengi.

Waziri WASSIRA amewaambia wabunge kuwa kwa muda wa miaka 11 tangu mpango huo uanze tayari umewafikia wakulima katika vijiji 15 na kusisitiza kuwa serikali itahakikisha inawafikia wananchi kupitia watendaji wa wilaya.

Aidha katika majibu yake kwa mbunge wa IRINGA MJINI,Mch. PETER MSIGWA waziri amesema  kuwa kufanikiwa kwa mpango huo kutategemea watendaji wa wilaya na kusisitiza kuwa  ‎endapo  mpango huo utakamilika wakulima watapata fursa za kukopa ili kuendeleza kilimo.


Related

Habari 4020381637234877628

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item