MAWASILIANO YA WENGER KUCHUNGUZWA

Arsene Wenger huenda akakabiliwa na hatua zaidi za nidhamu kutoka Uefa baada ya kuthibitishwa mawasiliano yake na benchi la ufundi la Ar...

Arsene Wenger huenda
akakabiliwa na hatua zaidi za
nidhamu kutoka Uefa baada ya
kuthibitishwa mawasiliano yake
na benchi la ufundi la Arsenal
yanachunguzwa.
Wenger alikuwa akitumikia
adhabu ya kutokaa kwenye
benchi la timu hiyo wakati wa
mechi ya kufuzu kwa Ubingwa
wa Ulaya dhidi ya Udinese.
Arsenal ilikuwa inahisi Wenger
huenda angeruhusiwa kupitisha
ujumbe kwa msaidizi wake Pat
Rice kwa kupitia kocha wa
kikosi cha kwanza Boro Primorac
Lakini Wenger alionywa wakati
wa kipindi cha mapumziko
kwamba hilo haliruhusiwi.
Uefa imethibitisha kwa BBC
kwamba wanachunguza kama
kulikuwa na uvunjaji wa kanuni.
Arsene Wenger alionekana
akikaa karibu na Primorac na
hakuhudhuria mkutano wa
waandishi wa habari baada ya
mechi, akisisitiza kuzuiwa kwake
kukaa kwenye benchi la ufundi
pia kunamzuia kufanya shughuli
na wanahabari.
Maafisa wa Arsenal
wameshangazwa na msimamo
huo wa Uefa, huku ikifahamika
wakati wa mkutano kabla ya
mechi kwamba Wenger
angeweza kutuma ujumbe kwa
jopo la makocha kupitia mtu wa
tatu ambaye ni Primorac.
Wenger kwa sasa hana budi
kusubiri iwapo Uefa wataona
mawasiliano yake na Rice kama
ni uvunjaji wa taratibu na
achukuliwe hatua, ingawa
wanaweza kukubali hiyo
inaweza kuwa ni matokeo ya
kutoelewa kuliko kwenda
kinyume na kufungiwa kwake
kukaa katika benchi la ufundi.
Meneja huyo wa Arsenal
kukatishwa tamaa kwake
kunaonekana kumeongezeka
baada ya timu yake kushindwa
kufunga mabao zaidi baada ya
kupata bao moja lililofungwa na
Theo Walcott.
Mara nyingi Udinese
walionekana wakiisumbua
Arsenal, lakini winga wa England
Walcott amesisitiza Arsenal
walikuwa katika "nafasi nzuri"
na wanakusudia kufanya vizuri
zaidi baada ya kuondokewa na
nahodha wao Cesc Fabregas
wiki hii.
Walinzi wa Arsenal Kieran Gibbs
na Johan Djourou waliumia msuli
wa paja wakati wa mechi hiyo.
Kwa sasa kuna wasiwasi iwapo
wataweza kucheza mwishoni
mwa wiki dhidi ya Liverpool,
huku Jack Wilshere naye akiwa
hajapona sawasawa kutokana
na kuumia kifundo cha mguu.

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item