BANDARI YA DAR ES SALAAM- BANDARI KUU UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi sita wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki utakaojadili masuala ya usafirishaji ...
https://mzukatz.blogspot.com/2015/03/bandari-ya-dar-es-salaam-bandari-kuu.html
TANZANIA
inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi sita wanachama wa jumuiya ya
Afrika Mashariki utakaojadili masuala ya
usafirishaji na uchukuzi.
Waziri wa
Uchukuzi nchini SAMUEL SITTA amewaambia waandishi wa habari jijini DAR ES
SALAAM kuwa katika mkutano huo utakaofanyika machi 26, marais sita kutoka nchi
hizo watazindua safari za treni ya mizigo kutoka Tanzania kupitia Rwanda ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo.
Waziri wa uchukuzi Samwel Sitta akizungumza na viongozi wa DRC kongo na waandishi wa habari jijini dsm leoPICHA:NA LIVINGSTONE MINJA |
Aidha waziri
SITTA ameongeza kuwa katika mkutano huo marais kutoka nchi za KENYA,BURUNDI,RWANDA,UGANDA,NA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO wakiongozwa na
rais JAKAYA KIKWETE wataafikiana masuala mbali mbali ya ushirikiano katika
sekta ya usafirishaji ikiwemo matumizi ya bandari ya Dar es salaam kama bandari
kuu kwa ukanda wa afrika mashariki na kati.
waandishi na washiriki mbalimbali wakufuatilia mkutano huo wa Mh. Sitta na viongozi wa KongoPICHA:NA LIVINGSTONE MINJA |
Sitta ameongeza kuwa katika mkutano huo marais kutoka nchi wanachama wa afrika mashariki na kati watazindua safari za treni ya mizigo kutoka TANZANIA kupitia RWANDA mpaka JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO katika kurahisisha usafirishaji wa mizigo baina ya nchi hizo.
waziri wa uchukuzi wa nchini drc Kongo Mh. Justin Kalumba Mwana ngongo PICHA:NA LIVINGSTONE MINJA |
Kwa upande
wake waziri wa uchukuzi kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya kongo Bw.JUSTINE
KALUMBA MWANA NGONGO ameipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada zake katika sekta ya
usafirishaji na kumshukuru rais JAKAYA
KIKWETE kwa kukubali TANZANIA kuwa wenyeji wa mkutano huo.