ZITTO KABWE ACT RASMI KADI NAMBA 7184... Ataja sababu ya kujiunga kwake
mwanachama mpya wa ACT bw.Zitto Kabwe akionesha kadi ya uanachama punde tu baada ya kuongea na waandishi leo PICHA NA :Livingstone Minja ...
https://mzukatz.blogspot.com/2015/03/zitto-kabwe-act-rasmi-kadi-namba-7184.html
mwanachama mpya wa ACT bw.Zitto Kabwe akionesha kadi ya uanachama punde tu baada ya kuongea na waandishi leo PICHA NA :Livingstone Minja |
mwanachama mpya wa ACT bw.Zitto Kabwe akionesha kadi ya uanachama punde tu baada ya kuongea na waandishi leo PICHA NA :Livingstone Minja |
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari na baadhi ya wanachama wa chama hicho katika hoteli ya serena jijini Dar es salaam katibu mkuu wa chama hicho taifa SAMSON MWIGAMBA amesema wamempokea ZITTO KABWE na wanachama wengine zaidi ya 15 wakitokea vyama mbalimbali vya siasa nchini.
bw.Zitto Kabwe akizungumza naandishi wa habari jijini dsm leoPICHA NA :Livingstone Minja |
Bw MWIGAMBA ameongeza kuwa ZITTO KABWE alijiunga na chama hicho jumamosi ya tarehe 21/03/2015 katika tawi la tegeta na kukabidhiwa kadi ya uanachama namba 7184 na mwenyekiti wa tawi hilo Bw.LUGANO MWAIKENDA huku akiongeza kuwa chama hicho kina dhamira ya kuleta maendeleo kwa taifa hivyo wamempokea kwa mikono miwili.
Kwa upande wake Bw.ZITTO KABWE amesema ameamua kujiunga na chama hicho kinachoendana na kile alichokipigania katika harakati zake akiwa mbunge kwani ni chama kinachokubaliana na misingi ya ujamaa huku akiahidi kufanya kazi na watu wote wenye kuamini siasa safi na za hoja .
imeandikwa na Praygod Thadey