UDSM yafanya kumbukizi kwa wanafunzi waliofariki katika ajali ya basi la MAJINJA EXPRESS... wasome hapa
Jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam imefanya ibada maalum ya kumbukizi kwa wanafunzi wake watano waliofariki dunia katika ajali ya ...
https://mzukatz.blogspot.com/2015/03/udsm-yafanya-kumbukizi-kwa-wanafunzi.html
Akizungumza katika ibada hiyo mkuu wa chuo cha fani za jamii profesa BELTRAM MAPUNDA amewataja wanafunzi hao kuwa ni ERICK KILEO,DAUD SOSTEN,JEREMIA WATSON na DIDIMO CHIWANGU wote wakiwa ni wanafunzi wa mwaka wa tatu katika fani ya shahada ya sanaa na elimu pamoja na FRANK MBAULE ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika fani ya shahada ya sanaa na elimu ambao walikuwa njiani kurudi chuoni mara baada ya kumalizika kwa likizo fupi.
naibu makamu mkuu wa chuo YUNUS MGAYA |
Naye naibu makamu mkuu wa chuo hicho prefesa YUNUS MGAYA amesema kuwa
jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam imepata pengo kubwa kwa
kuwapoteza wanafunzi watano kwa mkupuo katika ajali hiyo na kutoa pole
kwa famuilia za marehemu hao huku akiwataka wanafunzi wa chuo hicho kuwa
na utaratibu wa kuandika majina yao halisi pindi wawapo safarini kwani
lolote linaweza kutokea.
Aidha kwa upande wake rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam GILBERT NELSON amesema wao kama wanafunzi wamesikitishwa na vifo vya wanafunzi wenzao na kusema kuwa jumuiya ya wanafunzi wa chuo hicho ilizipokea kwa mshtuko taarifa za vifo hivyo huku akitoa pole kwa wanafunzi wote wa chuo hicho
Raisi wa serikali ya wanafunzi DARUSO bw. GILBERT NELSON |