TAMKO LA LHRC JUU YA PICHA MBAYA MITANDAONI

mashirika yanayofanya kazi za utetezi wa haki za binadamu hasa zile zinazohusumakundi maalumu yakiwemo wanawake wazee na watoto kwa pamoja ...

mashirika yanayofanya kazi za utetezi wa haki za binadamu hasa zile zinazohusumakundi maalumu yakiwemo wanawake wazee na watoto kwa pamoja leo wametoa tamko la kukemea vitendo viovu na udhalilishaji vinavyokiuka haki za binadamuna utu wao kupitia mitandao ya kijamii, simu za mikononi na hata kwenye vyombo vya habari.
Mkurugenzi wa Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) akizungumza na wanahabari ofisini kwao
akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya mashirika hayo Mkurugenzi wa Kituo cha haki za binadamu na sheria Bi Helen Kijo Bisimba amesema katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na vitendo vya baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii kusambaza picha za watu waliojeruhiwa vibaya katika ajali za magari, moto na kadhalika kitendo ambacho amekisema ni ukiukwaji wa haki za binadamu.


Aidha wameziomba taasisi zote za kijamii, kidini na kiserikali kutoa elimu kwa watanzania kuepukana na matumizi mabaya ya mitandao na kujali utu wa kila mtu katika jamii.
baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo
baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo
Jengo la kituo cha sheria na haki za binadamu








Related

Habari 2368486394332989810

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item