HII HAPA HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU Jangwani-Dar

HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU Ja...


HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015
Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu
1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini na tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.
2. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi.
3. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
a. Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.  
b. Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama elimu, afya, maji na makazi.
c. Mabadiliko ya kuondoa umaskini.
d. Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za maisha.
4. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa linakuwa.
5. Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na barabara bora zinajengwa.
6. Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa. Wanataka makazi bora.  
7. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga inahitimishwa.
8. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji.
9. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya sera za utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote ni wahanga wa siasa na sera hizi.
10. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka
11. Tusidanganyike, CCM hawana jipya
12. Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha ya wananchi.
13. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma. Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa wananchi wa kanda ya ziwa wanapata maji safi.
Ndugu watanzania
14. CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.
15. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa mikakati sahihi na siyo nadharia.
16. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa sekta bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji wa sera za kila sekta utakao leta maendeleo.
17. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini utakuwa na nguzo tano:-
a. Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
b. Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji
c. Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge.
d. Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira
e. Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.
18. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:-
1. Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri  na ushindani katika soko la ajira.
2. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata.
3. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini.
4. Kuimarisha  taaluma na mitaala katika mashule.
5. Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za wanafunzi.
6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa  ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafiri na zana za teknolojia.
7. Kufuta michango ya maabara ya shule za kata

AFYA
1. Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii
2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga kupunguza gharama za tiba.
3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki.
4. Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.
5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na nyumba na usafiri.
6. Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile serikali na hospitali za sekta binafsi.

ARDHI, MAJI NA KILIMO

1. Tutaimarisha  mfumo wa umiliki wa ardhi kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji.
2. Tutapima ardhi yote ya Tanzania na kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili kuipa thamani.
3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia ya kisasa na kumkomboa mkulima kutoka jembe la mkono.
4. Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
5. Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na kulinda vyanzo vya maji.
6. Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa wakulima elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na kujenga miundombinu husika.
7. Tutaweka mazingira rafiki yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji safi na salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa
8. Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa wakulima na wafugaji.
9. Tutasimamia kilimo cha biashara kinachozingatia maslahi ya nchi na  ya Watanzania.
10. Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao asilia ya Tanzania hususan mkonge.
11. Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.  

MIUNDOMBINU
1. Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya  Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
2. Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
3. Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya kisasa
4. Tutajenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
5. Tutajenga miundombinu ya kisasa na kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
6. Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano ya Watanzania
VIWANDA
1. Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu
2. Tutajenga viwanda vipya vya kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
3. Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano mali ghafi zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda

UCHUMI
1. Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii ambapo nguvu za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa mapato unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
2. Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za ndani kwa kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha mpito ili waimarike na waweze kuhimili ushindani. Tutawapa wafanyabiashara wetu upendeleo katika manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri ya biashara na kodi endelevu.
3. Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya biashara kwa masharti nafuu kabisa.
4. Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa Taifa.
5. Tutaimarisha sera ya ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia, kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye mitaji mikubwa bila kujali wanapotoka.
6. Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha mfumo wa Vyama vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na wakul

Related

Habari 213760923052126245

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item