Angalia Uzinduzi kampeni wa Chama Cha Mapinduzi CCM jijini DSM- full video
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amefungua pazia la kampeni za chama hicho kwenye Viwanja vya Jangwani katika tukio lililohudhuri...
https://mzukatz.blogspot.com/2015/08/angalia-uzinduzi-kampeni-wa-chama-cha.html
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amefungua pazia la kampeni za chama hicho kwenye Viwanja vya Jangwani katika tukio lililohudhuriwa na maelfu ya wananchi, huku akieleza mambo 25 atakayoyafanya iwapo Watanzania watamchagua kuwa Rais wa Awamu ya Tano.
Huku akitumia maneno: “Mimi kazi tu”, “Tanzania ya Magufuli ni ya
viwanda”, Dk Magufuli aliyetumia dakika 53 kueleza sera zake, kuanzia
saa 11.40 hadi 12.33 jioni alisema Watanzania wanataka kitabu kipya cha
mabadiliko na yeye na mgombea mwenza, Samia Suluhu ndiyo wanaoweza
kuyaletea.
Dk Magufuli ambaye ni Waziri wa Ujenzi, alizungumza lugha za makabila
saba kama ishara ya kuonyesha mshikamano wa Watanzania, huku makundi
mbalimbali kama madereva, mama lishe na mengine yaliyokuwapo uwanjani
hapo yakipaza sauti kutaka kusikia atawasaidia vipi akiingia Ikulu, ombi
ambalo mgombea huyo aliwajibu na kutuliza kiu yao.
Mgombea huyo wa urais wa CCM aliahidi kuanzisha mahakama maalumu ya
kusikiliza kesi za rushwa na ufisadi, kumaliza tatizo la wanafunzi wa
elimu ya juu kukosa mikopo, kuhakikisha mama lishe hawabughudhiwi,
kusimamia haki za wasanii, kulinda Muungano na usalama wa nchi.