Rais Omar al Bashir kupelekwa ICC?
Mahakama nchini Afrika Kusini imeahirisha kwa muda amri yake ya kumzuia rais wa Sudan Omar al Bashir, kuondoka nchini humo. Mahakama ita...
https://mzukatz.blogspot.com/2015/06/rais-omar-al-bashir-kupelekwa-icc.html
Mahakama nchini Afrika Kusini imeahirisha kwa muda amri yake ya kumzuia rais wa Sudan Omar al Bashir, kuondoka nchini humo.
Mahakama itasikiliza kesi hiyo tena Jumatatu ili kuamua ikiwa Bwana al-Bashir atakabidhiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC kukabiliana na mashtaka ya uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari yanayomkabili au la.
Rais huyo wa Sudan amekuwa nchini Afrika kusini kuhudhuria kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg. Waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Ibrahim al-Ghandour, amesema Bwana al-Bashir atarejea Sudan baada ya mkutano huo. "Tupo hapa kama wageni na kualikwa na serikali ya Afrika Kusini. Naamini serikali ya Afrika Kusini itaweza kukabiliana na mahakama zake na yeyote anayejaribu kumzuia Rais Bashir kuondoka nchini hapa. Naweza kuwaambia Rais Bashir ataondoka kwa wakati kama ilivyokuwa imepangwa." anasema waziri huyo wa mambo ya nje wa Sudan.
_BBC
_BBC