Sijawahi kulazimishwa na uongozi wa SIMBA kutumia uchawi _Sserunkuma

Mshambuliaji Dan Sserunkuma amesema yeye bado  ni mchezaji wa Simba na wala hafikirii kuondoka Msimbazi kwa sasa na hayo yote yanayosemwa d...

Mshambuliaji Dan Sserunkuma amesema yeye bado  ni mchezaji wa Simba na wala hafikirii kuondoka Msimbazi kwa sasa na hayo yote yanayosemwa dhidi yake ni uzushi.

Kumekuwa na habari kuwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa yuko kwao  Uganda aliuandikia barua uongozi wa klabu hiyo  kutaka kuvunja mkataba kutokana na kutoridhika na hali ya mambo ndani ya kikosi hicho hasa kuwekwa  benchi.

Sserunkuma ambaye aliikuwa  mfungaji bora kwa misimu miwili mfululizo kwenye Ligi Kuu Kenya akiichezea Gor Mahia yuko kwao Uganda kwa ruhusa maalumu akisumbuliwa na matatizo ya kifamilia.



Mganda huyo amefunga mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa anafuraha kuwa Simba na hajawahi kulalamika kubaguliwa ndani ya timu hiyo wala kusema anataka kuondoka hivyo hayo maneno yanayoibuka ni uzushi mtupu.

“Napenda kusema yafuatayo, ninafuraha kuwa Simba, Sijawahi kulalamika kubaguliwa ndani ya timu hiyo, Sitaki kuondoka Simba,  Sijawahi kulazimishwa na uongozi kutumia uchawi kama ambavyo siamini,” aliandika  Sserunkuma.

Sserunkuma alisema hajawahi kuambiwa na uongozi wa juu wa timu hiyo kutumia ushirikina kama wengi wanavyozusha kwani haamini mambo hayo kutokana na imani yake ya dini.  Naye wakala wa mchezaji huyo Ken Joseph alisema Sserunkuma bado mchezaji wa Simba mpaka mkataba wake utakapomalizika  mwaka 2016.

 “Ninachojua hakuna tatizo lolote kati ya Sserunkuma na uongozi wa Simba, alipewa ruhusa aende Uganda kushughulikia matatizo ya kifamilia, hivyo hajaniambia lolote kuhusu kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo, hivyo sifikirii kama hayo yanayozushwa ni ya kweli,” alisema Joseph.



_MWANANCHI

Related

Burudani/Michezo 7740047658153042464

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item