Kuelekea siku ya kifua kikuu duniani... Wizara ya Afya yasema haya...
Watanzania wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao katika vituo mbalimbali vya afya nchini katika maadhimisho ya siku ya kifua ki...
https://mzukatz.blogspot.com/2015/03/kuelekea-siku-ya-kifua-kikuu-duniani.html
Watanzania wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao katika vituo mbalimbali vya afya nchini katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yanayotarajiwa kufanyika kesho tarehe 24/03/2015 duniani kote ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’IBUA,TIBU,PONYA KILA MGONJWA WA TB’’
Hata hivyo Bw.DONALD amesema kuwa amesema kuwa kifua kikuu ni miongoni mwa magonjwa angamizi hapa nchini na kusema kuwa wadau wa afya nchini wanaongeza uchunguzi wa kutambua wagonjwa zaidi wa kifua kikuu nchini .
Aidha ameongeza kuwa kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza na unasababishwa na vimelea aina ya bacteria wanaojulikana kama mycobakteria huku akisema kuwa utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 30 ya vifo vya walioathirika na ugonjwa wa ukimwi vinatokana na kifua kuu.
Kwa upande wake meneja mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma nchini Dokta BEATRICE MUTAJOBA amesema kuwa matokeo ya tiba ya kifua kuku nchini ni mazuri kwa wagonjwa wengi ambapo zaidi ya asilimia 40 ya wagonjwa wamepona kabisa ugonjwa huo huku akiwataka watanzania wenye dalili za ugonjwa wa kifua kikuu kujitokeza na kuwahi kupata huduma kwa haraka zaidi.
Hata hivyo Bw.DONALD amesema kuwa amesema kuwa kifua kikuu ni miongoni mwa magonjwa angamizi hapa nchini na kusema kuwa wadau wa afya nchini wanaongeza uchunguzi wa kutambua wagonjwa zaidi wa kifua kikuu nchini .
Aidha ameongeza kuwa kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza na unasababishwa na vimelea aina ya bacteria wanaojulikana kama mycobakteria huku akisema kuwa utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 30 ya vifo vya walioathirika na ugonjwa wa ukimwi vinatokana na kifua kuu.
meneja mpango wa taifa wa kuthibiti kifua kikuu nchini Dk BEATRICE MUTAJOBA PICHA:LIVINGSTONE MINJA |
_imeandikwa na Praygod Thadey