Al-Shabaab yaungana rasmi na al-Qaeda

Kundi la Waislam wenye itikadi kali nchini Somalia, al-Shabaab, limetangaza kuwa linaungana na kundi la al-Qaeda. Tamko hilo limetolewa kat...

Kundi la Waislam wenye itikadi kali nchini Somalia, al-Shabaab, limetangaza kuwa linaungana na kundi la al-Qaeda.
Tamko hilo limetolewa katika picha ya video iliyotolewa na makundi hayo mawili.
Yusuf Garaad wa Idhaa ya Kisomali ya BBC ambaye ameitazama video hiyo amesema kundi hilo ambalo jina lake kamili ni Harakat al Mujahiddin al Shabaab, limetangaza rasmi kuungana na al-Qaeda.
Madai ya muungano huo yametolewa na kiongozi wa al-Shabaab, Ahmed Godane, au maarufu kama Abu Zubair.
Akizungumza kwa lugha ya Kiarabu,Abu Zubair amesema sasa watatii maelekezo kutoka kwa kiongozi wa al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri.
Akizungumzia Marekani, Ahmed Godane amesema wakati wa dolapekee duniani- Marekani - sasa umefikia mwisho na kuwa utawala wa Uislam ndio utachukua mamlaka.
Kiongozi wa al-Qaaeda, Ayman al-Zawahiri, ambaye pia ameonekana katika video hiyo, ameisifia al-Shabaab na kukiri na kukubali kwa kundi hilo kuungana na al-Qaeda.
Amesema hizo ni habari njema kwa wafuasi wake.
Wapiganaji
Al-Zawahiri amesema Somalia itakuwa ngome ya Jihad katika pembe ya Afrika na kuongeza kuwa watateketeza kile alichotajakuwa ni kiburi cha majeshi ya Kikristo kutoka Marekani, Ethiopiana Kenya dhidi ya Wasomali.

Post a Comment

emo-but-icon

Recent Post

Comments

Hot in week

My Blog List

Recent

item