Hawa ndio Nyota Wakali walioshindwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
Mafanikio ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yapo mbali kwa Zlatan Ibrahimovic, licha ya kucheza Barcelaon, Inter, Juventus, Milan na...

http://mzukatz.blogspot.com/2015/03/hawa-ndio-nyota-wakali-walioshindwa.html
Mafanikio ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yapo mbali kwa Zlatan Ibrahimovic, licha ya kucheza Barcelaon, Inter, Juventus, Milan na sasa PSG.
Kama alivyo mshambuliaji huyo, kipa mkongwe wa Italia, Gianluigi Buffon ana tuzo nyingi kwake, ikiwamo ya kutwaa Kombe la Dunia, lakini hakuwahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Swali ni je, kuna muda wa kutosha kwa kipa huyu mwenye miaka 37 kuendelea kusaka taji hilo la Ulaya?
Fabio Cannavaro (beki)
Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia 2006 (Balon d’Or), naye anaingia katika mkumbo huu, licha ya kuzichezea Inter Milan, Juventus na Real Madrid.
Tangu alipotwaa Kombe la Dunia akiwa na Italia ilimaanisha kuwa ameshachoka.
Sol Campbell (beki)
Beki huyu wa kati, ambaye ameichezea timu ya Taifa ya England michezo 73, alifanikiwa kufika fainali pekee ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Arsenal aliyoitumikia kwa misimu mitano, lakini Gunners ilichapwa mabao 2-1 na Barcelona mjini Paris.
Campbell alianza kwa kuifungia Arsenal katika mchezo huo, akimalizia kwa ustadi mkwaju wa adhabu uliopigwa na Thierry Henry kabla ya Barca kutoka nyuma na kuibuka na ushindi.
Lothar Matthaus (kiungo)
Katika wachezaji wote hao, Matthaus pia alikaribia kulitwaa taji hilo.
_mwananchi